Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuwasili Tunisia leo kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alitangulia Tunisia
Nabi ni raia wa Tunisia, Yanga imenufaika nae kwani anafahamu mazingira na siasa ya soka la Tunisia
Akiwa Tunisia, Nabi amepata nafasi ya kuwasoma US Monastir ambapo juzi alishuhudia mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Ben Guerdane ambao Monastir walifungwa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani
Leo Nabi atashuhudia mchezo mwingine ambao Monastir wanacheza dhidi ya Rejishe ugenini
Yanga itawasili Tunisia majira ya mchana ambapo kikosi kitakuwa na siku tatu za kujifua kabla ya kuwakabili Monastir siku ya Jumapili
Kuelekea mchezo huo, Yanga haina presha kubwa kwani hii ni mara ya pili kutua Tunisia katika michuano ya kombe la Shirikisho
Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Club Africain katika uwanja ambao watacheza na US Monastir, unawafanya Yanga wasiwe na hofu yoyote