Viingilio mchezo dhidi ya TP Mazembe mapemaaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2023
Viingilio mchezo dhidi ya TP Mazembe mapemaaa

Wakati Yanga ikitarajiwa kusafiri leo kuelekea Tunisia wakipitia Dubai tayari kwa mchezo wa kwanza wa makundi kombe la Shirikisho barani Afrika, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ametangaza viingilio kuelekea mchezo wa kwanza wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Februari 19 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni Wananchi Super Sunday, Kamwe amesema dhamira yao ni kuona wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa na kuhakikisha wanashinda mchezo huo na nyingine mbili zitazofuata ili kufikia malengo ya kutinga robo fainali

"Historia inaonyesha hatukuwa na matokeo mazuri kwenye hatua ya makundi katika miaka ya nyuma lakini msimu huu tuko tayari, tumedhamiria kufanya vizuri na kutinga robo fainali"

"Tunataka mashabiki wetu wawe na utamaduni wa kununua tiketi mapema ndio maana tumetangaza bei za vingilio vya mchezo wetu wa kwanza nyumbani dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Jumapili, Februari 19"

"VIP A ni Tsh 30,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/-, VIP C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 3,000/- kama utanunua tiketi yako sasa na Tsh 5,000/- kama utanunua tiketi siku ya mchezo"

"Tunajua umuhimu wa alama tisa katika mechi za nyumbani hivyo tunaanza na TP Mazembe, ni lazima tuhakikishe alama zote tatu zinabaki," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’