Mshambuliaji wa Yanga kinara wa mabao Obrey Chirwa ni miongoni mwa wachezaji wanaokosekana kwenye kikosi cha Yanga kinachoivaa Ndanda FC kutokana na majeruhi.
Chirwa ambaye yuko kwenye nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa upachikaji mabao akiwa na mabao 11, aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji.
Chirwa tayari amekosa michezo miwili dhidi ya St Louis, ligi ya mabingwa na Majimaji, kombe la FA lakini huenda akawa tayari kuivaa Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa March 06.
Mbali na Chirwa, kiungo Thabani Kamusoko(hayuko fiti), Donald Ngoma na Amissi Tambwe imeelezwa kuwa nao bado ni majeruhi.
Wengine majeruhi ni Abdalla Shaibu 'Ninja', Andrew Vicent chikupe na Yohana Nkomola.
Nahodha Nadir Haroub alipata msiba wa kufiwa na mwanawe wiki iliyopita naye bado hajarejea kikosini kutoka na udhuru huo.

ADVERTISE HERE