Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amethibitisha kuwa watamkosa winga Bernard Morrison kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya US Monastir
Mchezo huo utapigwa mwishoni mwa wiki hii huko nchini Tunisia
Nabi amesema ni pigo kwa Yanga kumkosa Morrison katika mchezo huo lakini nafasi yake itazibwa
"Sioni uwezekano wa Morrison kusafiri na timu, nafikiri huyo ndio mchezaji tunayeweza kumkosa katika safari hii lakini nafasi yake itazibwa"
"Kuna mpango tumeshaanza kuufanyia kazi jinsi ya kutafuta mtu muafaka wa kuziba nafasi yake na anaweza kuwasapraizi watu siku ya mchezo wetu wa kule," alisema Nabi
Yanga inatarajiwa kusafiri mapema wiki hii kuelekea Tunisia ili kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya mchezo huo ambao utapigwa Jumapili, Februari 12 katika uwanja wa Stade Olympique Hammadi Agrebi