Yanga imekuwa timu ya kwanza msimu huu kushinda mechi tisa mfululizo katika Ligi Kuu ya NBC. Mara ya mwisho kupoteza mechi ni dhidi ya Ihefu Fc, Novemba 29, 2022
Tangu wakati huo Yanga imeshinda mechi zake zote kuanzia mwezi Desemba, na kisha kushinda mechi mbili za Januari 2023 na leo imeshinda mchezo wa tisa mfululizo ikiwa ni dhidi ya Namungo Fc
Yanga imevunja rekodi ya Azam FC iliyoiweka msimu huu ya kushinda mechi nane mfululizo. Ukiongeza na ushindi wa mechi mbili za FA, Yanga imeshinda mechi 11 mfululizo

ADVERTISE HERE