Kama bado hujakamata tiketi yako hakikisha unaiweka mikononi mwako mda huu ili ifikapo saa 12:30 jioni uwe miongoni mwa mashabiki kindakindaki wa Yanga ambao watakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao katika mchezo dhidi ya Namungo Fc
Ni mchezo muhimu kwa Yanga kuzipata alama zote tatu ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Baada ya mchezo huu, Yanga itashuka tena uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya wiki mbili kumenyana na TP Mazembe katika mchezo wa kombe la Shirikisho, hatua ya makundi


ADVERTISE HERE