Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga leo watakuwa na nafasi ya kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi pale watakapoikabili Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kurudisha gap la pointi dhidi ya watani zao Simba kuwa sita
Jana Simba ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida BS na hivyo kufikisha alama 53 wakati Yanga ikiwa kileleni na alama 56
Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc haujawahi kuwa mwepesi, pamoja na Yanga kushinda mechi mbili za mwisho zilizokutanisha timu hizo
Katika misimu mitatu iliyopita, Yanga imeshinda mara mbili tu dhidi ya Namungo katika ligi kuu
Yanga imefanya maandalizi kabambe kuelekea mchezo huu, bila shaka kutakuwa na burudani ya aina yake uwanja wa Benjamin Mkapa
Kikosi cha kocha Nasreddine Nabi kimeongezewa nguvu baada ya baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi kurejea
Kiungo Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji hao ambapo Kocha Msaidizi Cedric Kaze jana alithibitisha kuwa Aucho atakuwa sehemu ya mchezo huo
Pia beki mpya Mamadou Doumbia yuko tayari kuanza mechi yake ya kwanza tangu alipotua Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo
Doumbia alitumika kwa dakika 45 kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers, mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 7-0
Mtanange utapigwa kunzia saa 12:30 jioni