Leo tumeianza safari ya mwezi Februar1 2023 ambao katika mwezi huu Yanga inatarajiwa kucheza mechi tano za mashindano
Mechi mbili ni Ligi Kuu na mechi tatu ni hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Safari inaaza Februari 04 siku ya Jumamosi kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Februari 12 kampeni ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho inaanzia ugenini kwa mchezo dhidi ya US Monastir ya Tunisia
February 18 Yanga itarejea jijini Dar es salaam kumenyana na TP Mazembe katika uwanja wa Benjamin Mkapa
February 22 ni mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao huenda ukapigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
February 26 Wananchi watasafiri nchini Mali kuwafuata Real Bamako katika mchezo wa tatu makundi Shirikisho
