Kazi nzuri inayofanywa mazoezini na beki mpya wa Yanga Mamadou Doumbia imemfanya Afisa habari wa timu hiyo Ali Kamwe atambe kuwa wameongeza chuma kingine kwenye safu ya ulinzi
Doumbia alitua nchini Jumamosi iliyopita na alianza kujifua na Yanga baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Wananchi watarajie kumuona mwishoni wa wiki hii kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers ambao utapigwa Januari 29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Yule beki wa CHAN (Doumbia) ni hatari sana, hacheki na mtu kabisa, yeye anapiga kazi tu, yaani anakwenda kuwaonesha balaa uwanjani, yule ni beki aliyekamilika, huku mazoezini anazima kila aina ya shambulizi, hivyo msubirieni uwanjani," alisema Kamwe
Doumbia ametua Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akichukua nafasi ya Gael Bigirimana ambaye mkataba wake ulisitishwa kwa makubaliano ya pande mbili
Yanga iliongeza wachezaji wanne katika dirisha dogo ambapo wachezaji wengine ni Metacha Mnata, Mudathir Yahya na Kennedy Musonda