Dozi ya mabao mengi itarejea kama zamani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jan 2023
Dozi ya mabao mengi itarejea kama zamani

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kasi ya kupachika mabao ya kikosi chake imeathiriwa na mabadiliko kadhaa

Aidha Nabi amewahakikishia Wananchi kuwa watarajie kuona mabadiliko katika mechi zijazo

Baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc, Yanga imeshinda mechi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, Ihefu Fc na Ruvu Shooting kwa ushindi wa bao 1-0

Nabi ametoa ufafanuzi wa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kuwa wachezaji wake walifanya mazoezi magumu kwa takribani wiki moja kabla ya mchezo huo

"Hatukupata nafasi ya kufanya maandalizi muhimu wakati wa kombe la Mapinduzi kama ambavyo wenzetu wengine hivyo ilikuwa lazima tutumie muda huu"

"Tukaona maandalizi hayo tungeyafanya katika hizi siku saba ambazo tulikuwa kambini, nafikiri ni vile watu wana kiu ya kuona timu inashinda kwa mabao mengi, tunawaelewa mashabiki kiu yao lakini wasiwe na haraka tunatengeneza msingi mkubwa wa hilo pamoja na mashindano ya CAF ambayo mechi zake hazipo mbali," alisema Nabi

Aidha Nabi amesema kuwa anaendelea kuboresha kikosi chake hasa baada ya usajili wa nyota wapya na mabadiliko katika eneo la kiungo baada ya Feisal Salum kuondoka

"Ukiangalia kuna kitu pale kati tunaanza kukitengeneza upya, kwasasa tuna viungo wengi huku baadhi ambao walikuwa wanacheza wakiwa majeruhi, tumelazimika kubadili mambo tukiwa pia na ujio wa Mudathir (Yahya) ambaye tunaendelea kumjenga taratibu"

"Hili linahitaji muda kidogo tukitafuta muunganiko wao mpya, tukasema pia tubadili mfumo pia kujaribu kutafuta muunganiko wa washambuliaji wa mbele tukicheza na washambuliaji wawili Musonda (Kennedy) na Fiston (Mayele).

"Yanga tuna timu bora lakini watu wasiwe na shida ya haraka kuona tunashinda kwa mabao mengi, jambo zuri ambalo vijana wanafanya ni kupigana kushinda, ndio lengo letu kuu ni kushinda, tutakuwa mabingwa kwa pointi nyingi kiujumla mengine yatafuata"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’