Wapinzani wa Yanga kwenye mchezo wa kombe la FA, Rhino Rangers wametamba kuwa watawasimamisha mabingwa hao watetezi katika mchezo utakaopigwa Jumapili, Januari 29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kocha wa Rhino Rangers Dani Mwan'gombe, ametamba kuwa wanakuja jijini Dar es salaam kuwapa mtihani mgumu Wananchi katika dimba la Mkapa
Mwan'gombe ametamba kuwa kikosi chao kina wachezaji wazoefu wlaiowahi kucheza ligi kuu hivyo hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo. Rhino Rangers inashiriki ligi daraja la pili
Wakati wao wakitamba, kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi makali Avic Town kujiandaa na mchezo huo pamoja na mechi nyingine za ligi na hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho
ADVERTISE HERE