Nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, wameifananisha Yanga na mwanariadha wa mbio ndefu anayeanza kushindana akikimbia taratibu, lakini mwisho wa siku anaibuka shujaa kwa wale ambao walitangulia mbele.
Abeid Mziba ‘Tekero’ aliyewahi kuichezea Yanga na Taifa Stars, alisema watetezi hao wa Ligi Kuu Bara waliuanza msimu huu vibaya kwa kujikongoja, ila kwa sasa wamekuwa watamu kiasi cha kusisimua mashabiki wa soka.
“Haikuaminiwa mwanzoni, lakini kwa siku za karibuni imezidi kushangaza wengi, mfano mzuri katika michuano ya kimataifa wengi walijua Yanga inaenda kupigwa ugenini kutokana na kupata ushindi kiduchu nyumbani, lakini ikawa tofauti,†alisema.
“Hata katika Kombe la FA, dhidi ya Majimaji Yanga ilitumia uzoefu wake kupenya robo fainali, hili ni jambo linalosisimua wengi.â€
Naye winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, alisema kwa namna Yanga ilivyokuwa inaonekana imechoka, iliwafanya Simba kuona kazi yao ni nyepesi, lakini mambo yapo tofauti.
Naye Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal ‘Bilo’ amesema inachofanya Yanga ni kama unavyosema usemi wa ‘Simba mwenda pole ndiye mla nyama’.
“Kitu muhimu Yanga ikiimarishe kikosi chake, wasije wakaona wanasifiwa na kuamini wapo vizuri sana, ila jinsi wanavyopata matokeo hata kwenye uchovu ni funzo kwa timu nyingine juu ya kuwa makini na timu hiyo kwa sasa,†alisema Bilo.
“Ina kikosi kinachopambana kwa ajili ya klabu, hilo ni jambo zuri.â€
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE