Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga leo majira ya saa 1 usiku watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuumana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi raundi ya 21
Mechi nyingine muhimu kwa Yanga kuwania alama zote tatu katika mkakati wao wa kutetea ubingwa wa ligi kuu
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wanahitaji kushinda mechi nane zinazofuata kwenye ili kujihakikishia ubingwa, hesabu ya mechi hizo inaanza leo katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Yaweza kuonekana kama itakuwa mechi rahisi kwa Yanga kutokana na mwenendo na nafasi ya Ruvu Shooting katika msimamo wa ligi, lakini mpira hauko hivyo
Ruvu Shooting wanaburuza mkia wakijikusanyia alama 14 kutoka mechi 20. Timu hiyo imeshinda mechi tatu pekee msimu huu na kutoka sare mechi tano
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanakwenda kuikabili Ruvu Shooting pasipo kuangalia nafasi yao kwenye msimamo wa ligi, kwani timu hiyo imewasumbua mara kadhaa walipokutana nayo
Mashabiki wa Yanga huenda leo wakamshuhudia beki wapo mpya Mamadou Doumbia ambaye alitua nchini siku ya Jumamosi