Kwa sasa mlinzi wa kulia wa Yanga Hassani Kessy yuko katika kiwango bora na hivyo kuwa chaguo la kwanza mbele ya rafiki yake Juma Abdul.
Kessy alirejea kikosini moja kwa moja kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC ambapo Yanga ililala kwa mabao 2-0 mkoani Mwanza. Aliingia baada ya Juma Abdul kuumia.
Michuano ya kombe la Mapinduzi ndio ikamuongezea uaminifu zaidi kutoka kwa benchi la ufundi ambalo sasa linamtumia kama mpishi wa mabao.
Katika mabao matatu yaliyofungwa na Yanga karibuni, Kessy amehusika kwenye mabao mawili.
Katika mchezo dhidi ya St Louis kule Shelisheli krosi yake ilitengeneza bao la Yanga lililofungwa na Ibrahim Ajib.
Pia juzi bao la pili dhidi ya Majimaji lilitokana na krosi yake mahiri iliyomaliziwa na Emanuel Martin.
Kessy ameongeza kujiamini na amekuwa akijituma pia kuhamasisha wenzake dimbani kila inapobidi.
Yanga ambayo sasa inawakosa idadi kubwa ya wachezaji wake muhimu kutokana na majeruhi inanufaika na uwepo wa wambanaji aina ya Kessy ambao wako tayari kuifia timu kuhakikisha inapata matokeo.
Juma Abdul amekuwa chachu ya mafanikio katika kikosi cha Yanga kwa misimu mitatu iliyopita.
Ushirikiano wake mahiri na winga Simon Msuva upande wa kulia ilikuwa chachu kubwa ya ubingwa wa Yanga misimu miwili iliyopita
Pengine kuondoka kwa Msuva na majeruhi mfululizo yameathiri kiasi kasi yake tuliyoizoea.

ADVERTISE HERE