Beki mpya wa Yanga Mamadou Doumbia amewasili nchini Alfajiri ya leo Jumamosi na kuungana na wenzake wanaoendelea kujifua Avic Town kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa Jumatatu, Januari 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kutua kwa beki hiyo akitokea Algeria ambako alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Mali inayoshiriki michuano ya CHAN
"Tumefurahi kumpokea beki wetu mpya, Mamadou Doumbia. Huyu ni beki bora ambaye sio kwamba atainufaisha Yanga tu, bali ujio wake utaongeza thamani ya ligi yetu," alisema Kamwe
Baada ya kukamilisha usajili wake na Yanga, Doumbia alipoteza sifa ya kushiriki michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi
Shirikisho la soka la Mali limempa baraka zote kusafiri nchini kujiunga na timu yake mpya, Yanga Sc