Mwanamuziki maarufu zaidi kwa sasa nchini Tanzania Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz ametangaza rasmi kujiunga na Yanga
Diamond Platinumz alitangaza uamuzi wake huo hapo jana katika hafla ya 'Birthday' ya Msemaji wa Yanga, Haji Manara iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na 'mastaa' mbalimbali, Diamond alikiri kuwa Manara ndiye aliyemshawishi kufuatilia masuala ya mpira wa miguu wakati yuko klabu ya Simba
Sasa kwa kuwa Manara tayari alishaondoka huko naye haoni sababu ya kuendelea kubakiΒ
Diamond alimpongeza Manara kwa ushawishi wake mkubwa katika soka la Tanzania, yeye amekuwa sababu ya watu wengi kupenda mpira wa miguu, hivyo naye ameamua kuungana nae katika klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE