Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga umesongezwa mbele na utapangiwa tarehe ili kuipa Muda klabu ya Yanga kufanya maandalizi ya mchezo wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Yanga itaivaa Township Rollers Marchi 06 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Sasa baada ya mchezo dhidi ya Ndanda FC kesho, Yanga itarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi ya Mabingwa.
Hii ni habari njema kwa klabu ya Yanga kwani ingekuwa katika mazingira magumu kama mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa umepangwa kupigwa March 03 usingeahirishwa.

ADVERTISE HERE