Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amefichua kuwa alimuhitaji kiungo Mudathir Yahya katika kikosi chake tangu msimu uliopita
Yanga ilimsajili Mudathir kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa juzi akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Azam Fc
Nabi ameeleza furaha yake kwa uongozi wa Yanga kufanikiwa kumsajili kiungo huyo fundi mwenye uwezo mkubwa wa kukaba
"Nimefurahi na nawapongeza viongozi wa Yanga kwa kufanikisha usajili huu. Mudathir nilimuhitaji kwenye kikosi changu tangu msimu uliopita lakini haikuwa rahisi kumpata, ujio wake nimeufurahia," alisema Nabi
Akizungumzia kiwango alichoonyesha katika mchezo dhidi ya Ihefu Fc, Nabi alisema Mudathir amecheza kwa asilimia 50% tu ya vile anavyotaka acheze hivyo anaamini ataendelea kuimarika na atakapofikia asilimia 100% mashabiki wa Yanga watafurahi
Mudathir alikuwa bora kwenye eneo la kiungo akionyesha umahiri katika kuzuia mashambulizi
Mudathiri huenda akatengeneza pacha bora na Khalid Aucho ambaye sasa atakuwa na uhuru wa kusogea mbele kuongeza mashambulizi wakati Mudathir akifanya 'kazi chafu'