Nabi apongeza wachezaji ushindi dhidi ya Ihefu Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2023
Nabi apongeza wachezaji ushindi dhidi ya Ihefu Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewapongeza wachezaji wake kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo mgumu wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc

Nabi amesema walifahamu mchezo huo ungekuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Ihefu Fc

Nabi amesema kwa uzoefu wake, anafahamu ni kawaida mechi ya kwanza baada ya mapumziko ya wachezaji huwa ni ngumu

Hata hivyo wachezaji walitimiza wajibu wao hasa kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kupata ushindi huo

"Nawapongeza wachezaji kwa ushindi huu. Mchezo haukuwa rahisi sio kwa sababu baadhi ya wachezaji hawakuwepo, tumecheza na timu iliyokuwa ikizuia zaidi. Ihefu Fc wana timu nzuri, wamefanya usajili mzuri ambao umewaongezea ubora zaidi"

"Mechi ya kwanza baada ya mapumziko ya wachezaji sio rahisi, lakini pia kwenye kikosi tulikuwa na wachezaji wapya ambao bado hawajawa kwenye muunganiko mzuri na wenzao"

"Baada ya mapumziko niliwaambia wachezaji wahakikishe wanakaa na mpira ili kuwachosha Ihefu Fc waliokuwa wanajilinda zaidi. Pamoja na mabadiliko tuliyofanya kwenye kipindi cha pili yalitusaidia kuongeza kasi ya mashambulizi na pengine tulistahili kufunga zaidi ya bao moja," alisema Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
40m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’