Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele leo amefunga bao la 15 katika ligi kuu ya NBC msimu huu
Mayele anahitaji kufunga bao katika mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting ili kufikia rekodi ya mabao 16 aliyofunga msimu uliopita
Msimu uliopita alihitaji mechi 30 kufunga mabao 16 lakini msimu huu amehitaji mechi 20 tu kufunga mabao 15
Katika historia ya ligi kuu, mfungaji bora wa muda wote ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga Mohammed Hussein 'Mmachinga' aliyepachika mabao 26
Katika mechi 10 zilizobaki, Mayele anahitaji kufunga mabao 11 ili kuifikia rekodi hiyo
Hakuna lisilowezekana msimu huu kwa Fiston Kalala Mayele...!
ADVERTISE HERE