Yanga imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Bao la Fiston Mayele katika dakika ya 64 lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo muhimu
Mayele alitumia makosa ya mlinda lango wa Ihefu Fc ambaye aliudondosha mpira chini ili auanzishe pasipo kufahamu Mayele aliyekuwa nyuma yake
Ni mchezo ambao kwa hakika Yanga haikuwa katika ubora wake lakini jambo muhimu zaidi ni alama tatu
Nyota wapya Mudathir Yahya na Kennedy Musonda waliitumikia Yanga kwa mara ya kwanza na hakika Wananchi wameridhishwa na kile walichokiona



ADVERTISE HERE