Metacha awaomba radhi Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jan 2023
Metacha awaomba radhi Wananchi

Mlinda lango Metacha Mnata amewaomba radhi mashabiki wa Yanga huku akiwaomba wampokee kwa mara ya pili wakati akirejea kutoka klabu ya Singida Big Stars

Metacha ambaye usajili wake umekamilishwa jana muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa kwa kuzingatia mahitaji ya benchi la ufundi, ameahidi kupambana ili kuhakikisha anatimiza malengo ya klabu na pia kuwapa furaha mashabiki

"Nikiwa kama mpambanaji nafahamu nilifanya makosa hapo nyuma, naomba mnisamehe na mnipokee. Metacha wa sasa sio yule wa nyuma, naahidi nitapambana ili kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri. Mimi ni Mwananchi na nitaendelea kuwa Mwananchi," alisema Metacha

Metacha amerejea Yanga kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu akitokea klabu ya Singida Big Stars, aliyojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Polisi Tanzania

Katika msimu huu akiwa na Singida Big Stars, Metacha amekusanya 'cleansheet' sita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’