Yanga imethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa mshambuliaji Heritier Makambo
Makubaliano ya pande mbili yamefikiwa Makambo akiondoka baada ya kutumikia miezi 18 ya mkataba wa miaka miwili ambao alisaini
Makambo alin'gara kwenye kikosi cha Yanga msimu wa 2018-19 na hata kusajiliwa na Horoya Ac aliyoitumikia kwa misimu miwili kisha kurejea tena Yanga msimu wa 2021/22
Hakuwa na wakati mzuri kwenye awamu yake ya pili, ni uamuzi sahihi kwa uongozi wa Yanga na hata kwake kwenda kutafuta changamoto mahali pengine
Mshambuliaji Kennedy Musonda aliyesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Power Dynamos ndiye aliyechukua nafasi yake
Kila la kheri Makambo, Wananchi hawatakusahau...!
ADVERTISE HERE