Yanga Princess wamesafiri hadi mkoani Dodoma ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa Jamhuri kupepetana na wenyeji wao Baobab Queens katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake, Serengeti Lite
Huenda ukawa mchezo wa kwanza kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Cuta Ninika aka 'Neymar' wa Msumbiji
Katika siku mbili alizofanya mazoezi na kikosi cha Yanga Princess, Cuta ameonyesha uwezo mkubwa, ni mchezaji ambaye hapana shaka ataiongezea makali safu ya ushambuliaji ya Yanga Princess
Utakuwa mchezo wa tano kwa Yanga Princess msimu huu ambapo katika mechi nne zilizopita, Princess wameshinda mbili, sare moja na kupoteza mchezo mmoja na hivyo kujikusanyia alama saba
ADVERTISE HERE