Yanga ilihitimisha kampeni michuano ya kombe la Mapinduzi jana usiku kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars hivyo kuondoshwa mashindanoni
Yanga ilihitaji kushinda mchezo huo ili kuweza kutinga nusu fainali
Katika kikosi kilichoshiriki michuano hiyo, kiliwajumuisha wachezaji wawili Yacouba Songne na Lazarus Kambole
Yacouba aliitumikia Yanga kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa ni majeruhi
Katika mechi mbili, Yacouba ameonyesha bado anastahili kuendelea kubaki kwenye kikosi cha Yanga
Pamoja na kuwa hayuko 'fit' kwa asilimia 100 lakini ameonyesha bado makali yake yapo

Aidha kwa upande wa Kambole waswahili wanasema 'hakuwa na maajabu' katika michuano hiyo
Hii ilikuwa nafasi muhimu kwake kuwashawishi benchi la ufundi kumrejesha kikosini lakini ni wazi hatma yake imebaki mikononi mwa kocha Nasreddine Nabi