Yanga kuivaa Majimaji yenye majanga leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Feb 2018
Yanga kuivaa Majimaji yenye majanga leo
Kikosi cha Yanga leo kinashuka kwenye uwanja wa Majimaji kuwavaa wenyeji wao Majimaji kwenye mchezo wa kombe la FA hatua ya 16 bora.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Majimaji Habib Kondo amethibitisha kusimamishwa kwa wachezaji saba wa timu yake wanaodaiwa kugoma wakishinikiza walipwe mishahara yao na fedha za usajili.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya wachezaji hawajalipwa mishahara yao kwa zaidi ya miezi mitatu. Kondo amesema kuwa amelazimika kuongeza wachezaji kutoka kikosi B

Hata hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya Yanga iuchukuliwe mchezo huo kwa wepesi kwani wakati mwingine inaweza kuwa ni mbinu tu ya kuwapoteza wapinzani.

Kwa kuwa mashindano hayo ni ya mtoano, hakuna muda wa kudharau mpinzani wako katika mazingira yoyote kwani jambo lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90.

Timu zote zinazoshiriki mashindano haya zina vikosi vipana. Aidha wachezaji vijana ndio wamekuwa chachu ya ushindi kwa timu nyingi msimu huu ikiwemo Yanga.

Mbali na Maji Maji na Yanga, mechi nyingine za ASFC leo ni Buseresere FC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na JKT Tanzania watakaomenyana na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi za 16 Bora ya ASFC zitakamilishwa Jumatatu ya Februari 26, Kiluvya United wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Stand United watakuwa wenyeji wa Dodoma FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’