Msafara wa wachezaji 25 wameondoka jijini Dar es salaam jioni kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Katika kikosi kilichoelekea Zanzibar, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amejumuisha wachezaji 13 wa kikosi cha kwanza na wachezaji 12 kikosi cha Yanga U20
Nabi amewajumuisha washambuliaji Yacouba Songne na Lazarus Kambole ambao hii itakuwa nafasi kuonyesha ni kwa kiasi gani wameimarika na utayari wao kurejea kikosini
Wachezaji waliosafiri ni Erick Johora(Golikipa), Hajji Mohamed Abassi(Golikipa )U20, Jacob Timothy Ipwaya(Golikipa) Bakari Nondo, Ibrahim Abdullah Bacca, Abdallah Shaibu Ninja na David Bryson
Wengine ni Maulid Kiakala(U20), Ally Said Mohamed (U20), Mohamed Omary(U20), Zawadi Mauya, Farid Mussa, Gael Bigirimana, Arafat Hussein(U20), Ahmed Fred Dennis(U20) na Crispin Ngushi
Pia wamo Maulid Tamila(U20), Yacouba Sogne, Dickson Ambundo, Clement Mzize, Lazarus Kambole, Nasri Ally Daud(U20), Raymond Ntaudyimara(U20), Daruwesh Rashid Ahmed(U20) na Shaibu Shaibu Mtita(U20).