Yanga imefunga mwaka 2022 kibabe kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro
Bao la mpira wa adhabu dakika ya 26 kutoka kwa guu la maajabu la Stephane Aziz Ki, limeihakikishia Yanga alama tatu muhimu katika mchezo ambao umeihakikishia Yanga kumaliza mwaka 2022 na ushindi unaowabakisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama sita
Ni msimu wa pili mfululizo Wananchi wanafunga mwaka wakiwa na alama 50 au zaidi
Licha ya kuwakosa takribani wachezaji watano wa kikosi cha kwanza, kwa mara nyingine Yanga imedhihirisha iko imara kama timu zaidi kuliko mchezaji mmoja mmoja


ADVERTISE HERE