Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wako mkoani Morogoro ambapo jioni ya leo majira ya saa 10 watashuka uwanja wa Manungu, Turiani kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Yanga inazisaka alama tatu muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Ni mechi ya kumaliza mwaka 2022, kila timu ikiwa imejipanga kumaliza mwaka kwa mafanikio
Yanga leo itashuka dimbani pasipo huduma ya baadhi ya wachezaji wake ambao watakosekana kutokana na sababu mbalimbali
Wachezaji majeruhi ni Khalid Aucho na Joyce Lomalisa wakati Djuma Shabani akiwa ni mgonjwa
Denis Nkane, Aboutwalib Mshery pia ni majeruhi wakati Bernard Morrison aliruhusiwa kusafiri Ghana kushughulikia matatizo ya kifamilia
Yanga inahitaji kushinda mchezo huu ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi