Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa winga Denis Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita baada ya kuvunjika mfup amdogo unaosababisha nyonga kujikunja
Nkane alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
Kulingana na ripoti ya daktari, Nkane atakuwa na vipindi viwili vya kuponya majeraha hayo
Kwanza atakuwa nje kwa wiki nne akiendelea na matibabu na baadae atakuwa na wiki mbili za kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuungana na wenzake
Nkane anatarajiwa kukosa mechi kadhaa za ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la Mapinduzi itakayoanza mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar
ADVERTISE HERE