Kulingana na Mwanaspoti, wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Majimaji wamejiengua na kususa kucheza mechi ya Kombe la FA dhidi ya Yanga ikielewa ni shinikizo la madai yao ya fedha za usajili na mishahara.
Kwa mujibu wa Kocha wa timu hiyo, Habibu Kondo mpaka jana asubuhi alikuwa amebaki na kikosi cha pili hivyo ikamlazimu kuongeza wachezaji wengine 14 kutoka timu yao ya vijana ili kuwawezesha kucheza na Yanga.
Akizungumza kwa sauti ya kukata tamaa, Kondo alisema changamoto hiyo inamuumiza akili na ilianza muda mrefu wachezaji kugoma, wengine wakafukuzwa na walioondoka kabisa kwenye timu.
Majimaji itaikaribisha Yanga kwenye mchezo wa kombe la FA hatua ya 16 kesho Jumapili, February 25 mchezo ukitarajiwa kupigwa kwenye dimba lao la Majimaji.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Yanga kushuka katika uwanja huo baada ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Lakini itakuwa mara ya tatu kwa timu hizo kukutana msimu huu ambapo katika mchezo wa mwisho Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.

ADVERTISE HERE