Yanga inapaa leo kwa usafiri wa Ndege kwenda Ruvuma tayari kwa mchezo wa kombe la FA (ASFC) unaopigwa kesho Jumapili dhidi ya Majimaji.
Yanga iliwasili juzi kutoka Shelisheli na uongozi kulazimika kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji kabla ya safari ya kwenda Ruvuma.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo wanakabiliwa na ratiba isiyo rafiki ambapo jana Afisa Habari wake Dismas Ten alisema walikuwa mbioni kufikisha malalamiko yao kwa Bodi ya Ligi.
Yanga inaomba angalau mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kupigwa March 03 usogezwe mbele ili ipate muda wa kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers unaopigwa March 06.
Baada ya kuivaa Majimaji kesho, Yanga itasafiri kwenda Mtwara kuivaa Ndanda FC February 28.
Licha ya ugumu wa ratiba hiyo, kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema kikosi chake kimejipanga kuibuka na ushindi dhidi ya Majimaji.
Γ’β¬ΕTutaenda kupambana, mchezo huu ni wa mtoano hivyo ni lazima tupambane, hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu na wao (Majimaji) watakuwa wamejiandaa,Γ’β¬Β amesema Nsajigwa.

ADVERTISE HERE