Winga Bernard Morrison leo huenda akapewa nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 2:15 usiku
Morrison alirejea kikosini hivi karibuni baada ya kupona majeraha ya nyama za paja ambayo yamekuwa yakimsumbua mara kwa mara
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimpumzisha katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union huku akicheza takribani dakika 45 katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao alitoa 'assist'
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Azam Fc uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2, Morrison alisababisha mkwaju wa penati ambao hata hivyo Djuma Shaban hakufunga
Hizi ni aina ya mechi ambazo Morrison hupenda kuzicheza na huwa na madhara makubwa
ADVERTISE HERE