Muda mchache baada ya Yanga kutoa taarifa kutotambua uamuzi wa kiungo Feisal Salum kuvunja mkataba, mchezaji huyo amewaaga rasmi Wanachama na Mashabiki wa Yanga
Ni wazi Feisal hayuko tayari kuendelea kuitumikia Yanga baada ya ofa nono ya Azam Fc
Bila shaka sasa Azam Fc watafuata taratibu kwa kukaa mezani na uongozi wa Yanga ili kumalizana
Ni sahihi Feisal hakufuata taratibu katika kuvunja mkataba na kwa kuwa amedhamiria kuondoka Yanga, ni wakati sasa wa Azam Fc kufika kunako meza ya mazungumzo
Kama jambo hili halitamalizwa kwa maridhiano ya pande mbili, ni wazi itakuwa ngumu kwa Azam Fc kumtumia Feisal
Ilikuwa hivyo kwa upande wa Yanga walipojaribu kumsajili Salum Abubakar 'Sure Boy' kwa mara ya kwanza
Aliandika barua ya kuvunja mkataba lakini viongozi wa Azam Fc wakaweka ngumu, ikashindikana Yanga kumsajili
Yanga walifanikiwa kumsajili baada ya Azam Fc kumsimamisha kwa muda mrefu na wakati mkataba wake ukiwa unaelekea ukingoni
Lakini pia hili linapaswa kuwa funzo kwa wachezaji, wahakikishe wanakuwa na watu sahihi ya kuwasimamia hasa kwenye masuala ya kimkataba ili kuepuka mikanganyiko ambayo inaweza kuwaweka nje
Wananchi hatuna kinyongo na Feisal tunamtakia kila la kheri, Yanga hii wamepita wengi, na watakuja wengi, wataondoka, Yanga itabakia
