Wananchi hawapaswi kuvurugwa na taarifa za kiungo wao pendwa Feisal Salum kuomba kuvunja mkataba wake ili ajiunge na Azam Fc
Kesho Wananchini wana mechi muhimu dhidi ya Azam Fc ambayo ushindi utaiweka Yanga kwenye nafasi nzuri katika mbio za ubingwa
Pengine jambo hili limefanywa wakati huu mahsusi ili kuivuruga Yanga kuelekea mchezo huo
Kocha Nasreddine Nabi ana kikosi imara ambacho hakijawahi kumtegemea mchezaji mmoja
Nabi ndiye aliyemtengeneza Feisal huyu anayen'gara, anao wachezaji wengi wa kuipa Yanga ushindi siku ya kesho
Ni kweli Feisal, ameandika barua ya kuomba kuvunja mkataba wake, kama masharti yote yamefuatwa, tusubiri taarifa ya uongozi na tutamtakia kila la kheri, Yanga ipo na itaendelea kuwepo
Walikuwepo wachezaji wazuri na waliopendwa sana lakini wakati ulipofika waliondoka
Kwa sasa macho ya mawazo yetu ni kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc hapo kesho..!