Kwa sasa Feisal Salum 'Fei Toto' ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri katika kikosi cha Yanga, hilo halina mjadala
Yaani Feisal yuko kwenye daraja moja akina Fiston Mayele kwa kuangalia mchango wake katika kikosi cha Yanga
Presha ni kubwa upande wake na hata kwa uongozi wa Yanga, jambo pekee ambalo Rais wa Yanga injinia Hersi Said anaweza kufanya ni kukubali kumuongezea mkataba na kuboresha maslahi yake mara dufu au kukubali asajiliwe na Azam Fc
Tetesi zimekuwa nyingi kiasi ambacho ni lazima Yanga iamue sasa kuhusu hatma ya Feisal
Azam Fc wamekuwa wakimuwinda Feisal kwa muda mrefu na walijipanga kutumia gharama yoyote kumsajili
Wanaamini kwa kumsajili Feisal watapata manufaa zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya klabu yao
Kwa wachezaji soka ndio kazi yao, hawapaswi kulaumiwa pale wanapochukua maamuzi ambayo wanaona yana maslahi kwao