Yanga yapania alama tatu dhidi ya Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Dec 2022
Yanga yapania alama tatu dhidi ya Azam Fc

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanajiandaa vyema kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc huku wakitambua mchezo huo hautakuwa mwepesi

Yanga inahitaji kupata ushindi dhidi ya Azam Fc ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za kuwania ubingwa

Mchezo wa mkondo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2 huku Yanga ikilazimika kusawazisha mabao mara mbili kupitia kwa Feisal Salum 'Fei Toto'

Kaze amesema wachezaji wanaonyesha juhudi mazoezini ikiwa ni ishara 'wanautaka' mchezo huo

"Tunatarajia mchezo mgumu na wa ushindani kwa sababu Azam FC ni miongoni mwa timu bora msimu huu wakiwa kwenye vita ya ubingwa"

"Mkakati wetu ni kuona hatuangushi pointi hata moja ili tujiimarishe kileleni lengo likiwa kutetea ubingwa. Tunawaheshimu Azam Fc kwani tunafahamu na wao wamejiandaa kwa ajili ya kushindana ili kuweza kufikia malengo yao pia," alisema Kaze

Yanga inakwenda kuchuana na Azam Fc kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa katika kiwango bora baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika michezo dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’