Ligi Kuu ya Wanawake Serengeti Lite imeingia mzunguuko wa tatu ambapo Yanga Princess leo itakuwa ugenini dhidi ya Simba Queens katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo huo ambao mashabiki watapata kuushuhudia pasipo kulipa kiingilio, utapigwa kuanzia saa 11 jioni
Ni dabi ya kwanza kwa kocha Sebastian Nkoma ambaye kabla ya kutua Yanga Princess aliwahi kuinoa Simba Queens
Katika Mkutano wake na wanahabari jana, Nkoma alisema anatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Simba Queens kwani ni timu anayoifahamu vyema na pia wao wanamfahamu
Lakini alisema dhamira ya Yanga Princess ni kushinda mchezo huo kwani msimu huu wana malengo makubwa ya kutwaa ubingwa
Kila la kheri Yanga Princess
ADVERTISE HERE