Mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa anaendelea kutengeneza mabao kwenye kikosi cha Yanga jana akiongeza assiti nyingine katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union
Krosi yake ilitua kichwani kwa Fiston Mayele ambaye mpira wake wa kwanza uligonga mwamba kabla ya kuwahi na kuuweka kimiani
Lomalisa amedhihirisha ubora wake na sasa amejihakikishia namba kwenye upande wa kushoto akimlazimisha Kibwana Shomari kurejea upande wa kulia ambako anabadilishana na Djuma Shaban
Lomalisa unaweza kumfananisha na mlinzi wa zamani wa Real Madrid Marcelo muda mwingi yuko nusu ya pili ya mpinzani
Unaweza kudhani ni winga lakini sio! ni uwezo wake wa kupanda kuongeza mashambulizi na kurudi nyuma kulinda pale timu inaposhambuliwa
Kutokana na umahiri wake, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine ana uhuru wa kutotumia winga katika upande anaocheza Lomalisa akimuachia majukumu yote yeye
Mchezaji ambaye hupangwa winga ya kushoto wakati mwingine huingia ndani kwenye eneo la kiungo pale timu inaposhambulia ili kumuacha Lomalisa amalize uwanja na kupiga krosi
Lomalisa amekuwa na ufanisi zaidi anapocheza na Farid Mussa upande wa kushoto, wawili hao wamekuwa wakipishana na kuongeza ufanisi timu inaposhambulia