Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wanakusudia kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Bodi ya ligi kuu ya Vodacom kuhusu ratiba ya michezo yake.
Mkwasa amesema kutokana na ukaribu wa michezo yao, wachezaji watakosa muda wa kupumzika na kuwa hatarini kupata majeraha zaidi na pengine kushindwa kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika michuano wanayoshiriki.
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya ligi kuu na bila shaka ataweza kusimamia malalamiko ya Yanga ambayo ni ya msingi.
Kwa mujibu wa ratiba, Yanga itacheza michezo mitatu katika kipindi cha wiki moja kabla ya kuivaa Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa jijini Dar es salaam.
Keshokutwa Jumapili, February 25 itakuwa Songea kuikabili Majimaji kwenye mchezo wa kombe la FA kisha kusafiri kwenda Mtwara kuikabili Ndanda FC kwenye mchezo wa VPL February 28.
Ikitoka Mtwara Yanga itakwenda mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar March 03, baadae inarejea jijini Dar es salaam kuivaa Township Rollers March 06.
Michezo hii ya mikoani iko karibu karibu mno. Ikumbukwe timu italazimika kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Ni dhahiri haitakuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi.
Mfano Yanga inacheza February 25 Ruvuma, February 26 itaondoka kuelekea Mtwara. Hapo itakuwa na siku moja ya kupumzika/kufanya maandalizi kabla ya kuivaa Ndanda FC Feb 28.
Hali kama hiyo itatokea watakapokwenda Morogoro na kisha kurejea Dar kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa.
Hali ni tofauti kwa watani zao wa jadi Simba ambao michezo yao miwili ya ligi kabla ya kuivaa Al Masry itapigwa jijini Dar es salaam.
Simba itacheza na Mbao FC Feb 26 kwenye uwanja wa Taifa kisha kuivaa Stand United March 03/04 katika uwanja huo huo.
March 09 Simba itashuka tena kwenye uwanja wa Taifa kuivaa Al Masry kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, kombe la Shirikisho Barani Afrika.

ADVERTISE HERE