Winga wa zamani wa Yanga Mrisho Ngasa amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kuonyesha kiwango bora katika mechi zao kwenye ligi kuu
Jana Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ngasa amekiri kuwa sasa Yanga inacheza mpira mkubwa pengine kuliko hata nyakati zile yeye akiwa mmoja wa wachezaji
Ngasa ametamba kama angekuwa kwenye kikosi hiki basi angekuwa na uhakika wa kufunga kwenye kila mchezo
"Hii yanga toka naijua Kwa sasa wanapiga mpira mkubwa. Kwa kipindi hiki ningekua nasema tu nisipofunga nipigwe mpaka nirefuke!"
"Kiukweli hongera wachezaji na benchi zima la ufundi kipindi hiki hata ile mechi ya muda TFF wamechanganya mngekuwa na timu hii kusingekuwa na mgomo wa muda Kwa sasa mna timu nzuri sana muda wowote mnauwezo wa kufunga Hongera zenu Enjoy soccer," aliandika Ngasa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
