Yanga 'kupaa' Ruvuma kesho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2018
Yanga 'kupaa' Ruvuma kesho
Kikosi cha Yanga SC kimerejea Dar es Salaam usiku wa jana kutoka Mahe, Shelisheli ambako katikati ya wiki kilikata tiketi ya kwenda Raundi ya Kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 na wenyeji, Saint Louis Suns United katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Uwanja wa Linite.

Mabingwa hao wa Tanzania wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya Februari 10 kushinda 1-0 pia Uwanja wa Taifa.

Yanga leo watafanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, kilichopo Kurasini mjini Dar es Salaam kabla ya mapema kesho kusafiri kwa ndege kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Jumapili.

Kwa kuitoa St Louis, Yanga itakutana na Township Rollers ya Botswana katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo nayo iliitoa El Merreikh ya Sudan.

Yanga SC wataikaribisha Township Rollers ya Botswana Machi 7 Uwanja wa Taifa, kabla ya kwenda Gaborone kwa mchezo wa marudiano, Machi 17.

Hatua ya 16 Bora ya ASFC itaendelea leo kwa Singida United kuwakaribisha Polisi Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida na KMC kumenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mbali na Maji Maji na Yanga, mechi nyingine za Jumapili ni Buseresere FC watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na JKT Tanzania watakaomenyana na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi za 16 Bora ya ASFC zitakamilishwa Jumatatu ya Februari 26, Kiluvya United wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Stand United watakuwa wenyeji wa Dodoma FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’