Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo anarejea kwenye benchi baada ya kukosa mechi tatu zilizopita akitumikia adhabu kutoka Bodi ya Ligi
Nabi leo ataiongoza Yanga katika mchezo muhimu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku
Ni mechi ambayo anakwenda kukutana na kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye sasa anainoa Polisi Tanzania
Kabla ya kutua Polisi Tanzania, Zahera alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la Vijana na Wanawake katika klabu ya Yanga
Mkataba wake ulimalizika mwezi Septemba 2022 na Yanga kuamua kutomuongezea na badala yake wakamteua Cedric Kaze kushika wadhifa huo pia akiendelea na majukumu yake ya kocha msaidizi wa Yanga
Baada ya kutoka Yanga, mara kadhaa Zahera amesikika akikosoa mbinu za Nabi pamoja na baadhi ya wachezaji hasa wakati wa mechi za CAF walizocheza Yanga dhidi ya Al Hilal na Club Africain
Leo ni siku ya kipekee kwa Nabi kumdhihirishia Zahera kuwa hakuitwa Profesa kwa bahati mbaya, ni kutokana na ubora wa mbinu zake uwanjani