Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amemkaribisha Kocha Mwinyi Zahera katika uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi ambako mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania utapigwa
Zahera ndiye kocha mkuu wa Polisi Tanzania aliyojiunga nao hivi karibuni
Wengi wanakumbuka baada ya Yanga kutoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Club Africain katika mchezo wa kwanza kombe la Shirikisho hatua ya mtoano,Β Zahera ni miongoni mwa waliokosoa sana akidai baadhi ya wachezaji Yanga wamenenepa akimlenga Djuma Shabani
Kamwe amesema wanamkaribisha Zahera dimba la Mkapa Jumamosi na watavaa jezi zao nyeusi ili wamuoneshe jinsi walivyonenepa!
ADVERTISE HERE