Yanga haitarajiwi kufanya usajili mkubwa katika dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa usiku saa sita na dakika 1 kuamkia kesho Ijumaa
Hilo limethibitishwa na Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ambaye amesema kikosi chake kiko imara, maboresho yatafanyika kwenye nafasi chache zenye mapungufu
Nabi amependekeza usajili wa wachezaji watatu katika nafasi za beki wa kati, mshambuliaji mmoja na kiungo mkabaji.
"Hatuitaji kufanya usajili wa wachezaji wengi sababu bado tuna timu nzuri ya ushindani hao wachezaji watatu ambao tumepanga kuwaongeza kwenye dirisha dogo ni kwa ajili ya kuziba sehemu zilizoonesha mapungufu kwenye mechi za mtoano na ligi," Nabi amenukuliwa na SpotiLeo
Yanga imedhamiria kutetea taji la ligi kuu, FA na kuvuka hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwa imepangwa kundi D na timu za TP Mazembe, US Monastir na Real Bamako