Baada ya kucheza kwa dakika zote 90 kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Kurugenzi Fc, mlinda lango Erick Johora amesema anaamini wakati wake wa kupata nafasi ya kucheza umefika
Johora hakuwa na kazi kubwa ya kufanya katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 8-0
Johora aliyesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya Aigle Noir ya Burundi, huenda akapata nafasi zaidi katika mechi zinazofuata hasa baada ya mlinda lango namba mbili Aboutwalib Mshery kupata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa mwezi mmoja
Mwenyewe amesema yuko tayari kutekeleza vyema majukumu yake na kuhakikisha anaisaidia timu
"Nilikuwa na imani wakati wangu utafika, nafurahi kuona nimeisaidia timu yangu katika mchezo dhidi ya Kurugenzi"
"Kufanya kazi kwa bidii mazoezini ndio kitu pekee ambacho nilikuwa nikiweka juhudi kwa sababu niliamini kuna siku nitapata nafasi, naamini kuwa huu ni mwanzo wa kuendelea kupata nafasi zaidi ya kucheza"
"Nimekuwa na uhusiano mzuri na makipa wenzangu. Tumekuwa tukifanya kazi kwa ushirikiano, sote tupo hapa kwa ajili ya Yanga na hilo ndilo jambo muhimu kwetu kuliko masuala binafsi, mchango wa kila mchezaji ni muhimu kwenye timu," alisema