Yanga kuendeleza moto wa ushindi FA, VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2018
Yanga kuendeleza moto wa ushindi FA, VPL
Baada ya kufuzu raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea leo Alhamisi saa tatu usiku kisha kujiandaa na safari ya mkoani Ruvuma kuivaa Majimaji kwenye mchezo wa kombe la FA.

Mchezo dhidi ya Majimaji unatarajiwa kupigwa Jumapili, February 25, 2018.

Ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya St Louis ya Shelisheli umeongeza ari kwa wachezaji wa Yanga ambao wameahidi kuendeleza moto huo katika ligi na kombe la FA.

"Tulichokuwa tunakitaka tumekipata kwa hiyo wanayanga waendelee kutuunga mkono wasikate tamaa kwa mechi zijazo. Tumeshatoka hatua moja tumeenda nyingine, sasa tunarudi kwenye ligi," Hassani Kessy alifunguka baada ya mchezo wa jana.

Hata hivyo Yanga inakabiliwa na 'ratiba isiyo rafiki' kutokana na ushiriki wake katika michuano mingi.

Yanga ndio timu pekee inayoshiriki michuano mitatu kwa mpigo yaani ligi ya VPL, kombe la FA na ligi ya Mabingwa.

Kwa kuwa TFF imesema msimu huu haitaruhusu timu moja kuwa na zaidi ya mchezo mmoja wa kiporo, Yanga inalazimika kukabiliana na ratiba iliyosheheni michezo iliyo karibu karibu.

February 25, 2018
Majimaji vs Yanga (FA)

February 28, 2018
Ndanda vs Yanga (VPL)

March 03, 2018
Mtibwa Sugar vs Yanga (VPL)

March 06, 2018
Yanga vs Township Rollers (CAF CL)

Kwa mujibu wa ratiba, Yanga inakabiliwa na michezo mitatu ya mikoani kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kuivaa Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa.

Ikitoka Ruvuma Yanga itasafiri kwenda Mtwara kuivaa Ndanda FC, kisha itakwenda mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar kabla haijarejea jijini Dar es salaam.

Michezo yote inatofautina kwa wastani wa siku tatu tu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’