TP Mazembe ndio klabu inayoonekana kuwa tishio zaidi kwenye kundi D michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Ni kutokana na uzoefu na mafanikio waliyonayo katika michuano ya CAF katika misimu ya hivi karibuni
Lakini pia katika kundi D, wamo US Monastir kutoka Tunisia. Hawa ndio waliwaondosha mabingwa wa msimu uliopita RS Berkane katika michuano ya kombe la Shirikisho
Hii ni mara yao ya kwanza kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho lakini ni timu iliyojipanga kwelikweli, wana hela, pengine kikosi chao ndio chenye thamani kubwa zaidi kuliko wapinzani wake wote katika kundi D
Real Bamako sio timu ya kutisha sana, kule Mali timu zenye mafanikio zaidi ni Stade Malien na Djoliba AC hivyo ni timu ambayo inasaka mafanikio katika mashindano ya CAF kama ilivyo Yanga
Kitu cha kujivunia Yanga katika michuano hii ni ubora wa kikosi chake kilichosheheni wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya CAF
Lakini pia Yanga ina kocha Nasreddine Nabi ambaye amewahi kutwaa kombe la Shirikisho akiwa na AC Leopards ya DR Congo mwaka 2012
Yannick Bangala, Fiston Mayele, Jesus Moloko, Joyce Lomalisa, Tuisila Kisinda na Djuma Shaban hawawezi kuihofia timu kama TP Mazembe kwani wamecheza na kuifunga mara nyingi tu
Jambo la msingi kwa viongozi wa Yanga ni kuhakikisha wanafanya maboresho muhimu hasa katika eneo la ulinzi na safu ya ushambuliaji kwa kuongeza mshambuliaji mwenye daraja la Mayele au zaid