Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wamejipanga kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi
Jana droo ya hatua ya makundi ilifanyika huko Misri Yanga ikipangwa kundi D pamoja na klabu za TP Mazembe, US Monastir na Real Bamako
Kamwe amesema Yanga haiendi kushiriki tu michuanp hiyo, bali imejipanga kushindana
"Tumepangwa kundi D pamoja na timu ambazo kwa kiasi tuna taarifa zake. Tumeshacheza na TP Mazembe wakati flan katika michuano hii. Hawa Monastir ni timu ya mtaani kabisa anapotoka kocha wetu Nabi kule Tunisia"
"Mlinda lango wetu Djigui Diarra anazo taarifa za kutosha kuhusu wapinzani wetu wengine Real Bamako kutoka Mali"
"Kama alivyosema Mtendaji wetu Mkuu Andrea Mtine, katika michuano ya mwaka huu tumedhamiria kupeleka ujumbe Afrika, tumejipanga kushindana," alisema Kamwe