Mwenyekiti wa Kamati ya michuano ya kombe la Mapinduzi mwaka 2023 Khamis Abdullah Said ameeleza kwamba bajeti ya michuano hiyo msimu huu imeongezwa na inaweza kufikia Million 450
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Said alisema fedha zinazohitajika sio chini ya milioni 400 lakini wametenga bajeti ya Tsh Milioni 450
Aidha Mwenyekiti pia ametaja vilabu vitakavyoshiriki msimu huu kuwa ni kama ifuatavyo;
ZANZIBAR
- Kvz
- KMKM
- Malindi
- Mlandege
- Jamuhuri
- Chipukizi
TANZANIA BARA
- Yanga SC
- Simba SC
- Azam FC
- Singida BS
- Namungo FC
Klabu ya Aigor Noir ya Burundi imealikwa kushiriki michuano hiyo inatayoanza mwishoni mwa mwezi huu visiwani Zanzibar
ADVERTISE HERE